Jumapili iliyopita, wanahabari wa shirika la Standard Media – nikiwa mmoja wao – tulikuwa mjini Eldoret kupeperusha moja kwa moja makala ya 10 mashindano ya KASS MARATHON.

Jumapili iliyopita, wanahabari wa shirika la Standard Media – nikiwa mmoja wao – tulikuwa mjini Eldoret kupeperusha moja kwa moja makala ya 10 mashindano ya KASS MARATHON.

Baada ya mashindano hayo kukamilika, niliwaacha pembeni wahariri wenzangu Hassan Jumaa (KTN), Robin Toskin (Standard) wakibadilishana mawazo na washiriki.
Miye nikaitwa pembeni na mashabiki wengi tu wa Radio Maisha. Kilianza kikao cha watu 20, muda si muda ukawa mkao wa watu kama 100 hivi. Ungedhani naandaa makala ya GUMZO.
Tulianza kuangazia KASS MARATHON, kisha maoni mseto yakaijitokeza. Wananchi hao wengi wao hasa kutoka kaunti za Uasin Gishu, Nandi na Marakwet, walinituma.
Na mjumbe hauawi. (Nichukue nafasi hii kuwapa chamge mashabiki wote wa Redio Maisha walioko Bonde la Ufa.)
Mashabiki wangu hao waliniomba nitume salamu zao ‘kama barua’ kwa rais wa Jamhuri ya Kenya, Uhuru Muigai Kenyatta.
Pamoja na kwamba walishuku rais hasomi magazeti kwa kuwa yeye huyatumia “kufungia nyama”, wameomba wandani wake waisome barua hii na wampe ushauri kabla ya sherehe zake kubwa za taifa za mwisho wa mwaka huu mnamo Desembe 12, sherehe za Jamhuri.
Hii ni barua, japo si rasmi wala ya kirafiki!
“Sisi watu wa Bonde la Ufa twakuamkua Mheshimiwa rais. Tunayo maombi mengi ambayo tutakupa ukija huku na kutuhutubia katika viwanja vya huku ama hata kutusalimu barabarani.
Tutajitokeza kwa wingi tu katika mikutano yako ya hadhara na siasa. Hata hivyo, leo hii tumemtuma Hassan mwana wa Ali akuarifu yafuatato:
Kwanza kabisa, angalia bei za bidhaa muhimu. Ugali umekuwa ghali. Maziwa hata ndio usiseme rais wetu! Pili, kwa unyenyekevu, twakuomba upambane na ufisadi bila kukata tamaa.
Si jambo zuri vyombo vya habari kutawaliwa na taarifa za WIZI WIZI WIZI, mawaziri wako kuhojiwa kushoto kulia na TUME MAALUM!
Ufisadi katika serikali kuu umesambaa kama virusi hadi huku mashinani hivi kwamba baadhi ya magavana wetu wanajenga mabango barabarani kwa kima cha mamilioni ya pesa kukutajia tu baadhi ya skendo huku mashinani!
Hebu maliza uozo katika wizara ya michezo. Kwa sasa umesikia kuhusu mwanariadha wetu aliyetapeliwa na wakili ambaye ni spika huku kwetu. Hata hivyo, fanyia kazi ripoti ya uozo uliojiri huko Rio wakati wa mashindano ya olimpiki, Rio, Brazili.
Twakuomba rais.Tusikuchoshe sana maana twajua majukumu ni mengi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *